About Tanzania Students Connect

My photo
Tanzania Students Connect aims at connecting students from different higher learning institutions across the country and make this blog a place of change for youth and different matters of our concern in our lives, country and the world at large.

Saturday, April 30, 2011

UCHAGUZI UDOM CCM WAMEPANDIKIZA WAGOMBEA?


Ikiwa zimebaki siku chache kwa wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma(UDOM) kupata serikali mpya..tuhuma zimeendelea kuibuliwa kuwa chama tawala kinasuka uongozi wa Udom kwa maslahi ya chama hicho.

Katika Kitivo cha Sayansi za Jamii (Social Science) majina ya waliopitishwa kugombea u-raisi wa kitivo ni;

- Philipo Mwakibinga
- Godwin Gonde
- Israel

Tume ya uchaguzi pia imempitisha mtu mmoja tu kugombea nafasi ya makamu wa raisi Social sciences, japo walikuwa wagombea watatu.

Sifa kubwa ya kupitishwa ni kuwa mwanachuo tu, cha ajabu inaonekana kama kinyume cha demokrasia, au labda kuwekana. Waliopo madarakani ndo huwachagua watu wa tume ya uchaguzi, hivyo kuna hiyo possibility.

Na kuna uwezekano wa kuto tokea uongozi huru na bora UDOM kamwe, kwa upande wa federation pia mambo sio mazuri kwani tume imempitisha

- Mwesiga thobias;
Huyu jamaa ndio yule aliyetoa tamko kwamba CHADEMA waombe msamaha kwa kutoka nje wakati presidaa anahutubia.

- abubakar mohamed;
Huyu ni mdogo wake Bashe yule aliyewahi kuambiwa sio raia, ambaye ni mfanyakazi wa Rostam Aziz na kuna tetesi kuwa kapewa mil 5 na Bashe kwa ajili ya ku-take over uongozi.

- Deborah ( ) ambaye pia amekuwa akionekana katika mikutano mikubwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa wakati wa kampeni za JK.


Soon tutaongeza majina zaidi ya wagombea.


Ombi kwa  wasomo hawa ni kuchagua viongozi wenye sifa na bila kurubuniwa na vyama vya siasa ili picha ya Udom isiwe ya kisiasa bali ya kitaaluma.

TUNAWATAKIA UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA NA WA AMANI

No comments:

Post a Comment